BurudaniUncategorized

Nitakuwa muongo kusema Fella kaegemea WCB – Chege

Msanii wa Bongo Flava kutoka TMK, Chege amesema si kweli kuwa meneja wa kundi hilo Mkubwa Fella ameengemea zaidiWCB kwa sasa kuliko TMK.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Najiuliza’ aliyofanya na Ray C & Sanapei Tande, ameiambia Twenzetu ya Times Fm kuwa muziki umebadilika na meneja anapaswa kupanua wigo wake wa kazi.

“Hawezi kuengemea yeye pia ni meneja inabidi apanue wigo wake, mimi naona ni kitu sawa kwa sababu mimi sina mapungufu upande wangu kwake, kwa hiyo kama sina mapungufu nitakuwa mtu muungo kusema ameegemea WCB, sio kweli,” amesema Chege na kuongeza.

“Hawezi kunifikiria kuniacha au kumuacha Temba, hata afanye kazi na Jay Z Chege atabaki kuwa pale, Temba tabaki kuwa pale,” amesisitiza.

Mkubwa Fella amekuwa ni sehemu ya uongozi wa label ya WCB pamoja na Sallam na Babu Tale ambaye kipindi cha nyuma aliwahi kulalamikiwa na Tunda Man kuwa ameegemea zaidi katika label hiyo kuliko Tip Top Connection.

By Peter Akaro 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents