Habari

Njia 15 za kumfanya MTEJA awe TEJA wa huduma yako (2)

By Mark Rose Msemwa
Mpendwa msomaji, fahamu kwamba kila mtu ni sehemu ya biashara na biashara ni mtego; Anayetegwa ni mteja. mtego ni wewe na taaluma yako. Na chambo ni huduma yako. Huu ni muendelezo wa makala hii na leo tunaangalia njia nyingine tano.

SA-image-business-woman-2

6. Mjue mteja wako ni mtu anaependa nini, wengine hupenda utani, wengine siasa, muziki, utoto lakini pia wengine hupenda heshima na walichofuata tu, mimi nikiwa na baadhi ya wateja naonekana mcharuko, muda mwingine ni mtu mwenye hekima duniani hakuna, hii ni kutokana na ninavyowajua wateja wangu, the best way ni kuwa mpana habari za ndani na nje ili umudu aina za wateja wote.

7. Huu ni mwiko mwingine – Usimseme mteja mbele ya mteja mwingine au kwa mteja mteja mwingine hata akilianzisha tafuta njia sahihi ya kukwepe hilo. Kwa ukimsema mteja ambaye hayupo na huyu aliepo anajua asipokuwepo atasemwa tu.

8. Tunza mawasiliano ya mteja kiofisi kwa mawassiliano ya kiofisi tu, sio kwa mawasiliano binafsi au kutangazia shida zako, haifai itakuharibia no matter how good you are on what you are doing!! Si ushawahi kusikia “aah Ndimbwindambwa anajua kazi yake ila njaa kali, kwanini uambiwe hivyo? Jadili shida zako na boss wako.

9. Watakie heri ya sikukuu wateja wako kiofisi na huku ukiihusisha ofisi yako sio unataja jina lako, mteja hakujui kwa jina lako anakujua kwa taaluma na huduma yako tu. Pia ukihusisha jina lako kuna hatari ya kusababisha kero kwa baadhi ya wapendanao wanaosomeana text, e-mail nk.. Au hata mtoto kwa mzazi mchunguzi utamtia wazimu. (Ukitakie sikuku njema kibinti cha watu mwishoni
jina la kiume weeee).

10. Wape taarifa za mali mpya, punguzo la bei, kuhama kwa huduma yako n.k. Hii humfanya mteja ajione muhimu kama ukweli ulivyo……

Itaendelea……

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents