Habari

NMB na EFM za dhamiria kukusanya bilioni moja NMB Marathon

Benki ya NMB kwa kushirikiana na kituo cha redio EFM wamezindua rasmi msimu wa pili wa mbio za  hisani (NMB Marathon) tarehe 30/08/2022, ambapo kilele cha msimu huu kinatarajia kuwa tarehe 24/09/2022 viwanja vya Leaders club Kinondoni jijini Dar es Salaam, huku ikiwa na kauli mbiu  ya ” mwendo wa upendo “ikiwa na  lengo na mikakati endelevu kwa ajili ya kuimarisha sekta ya afya.

Akizungumza kaimu mkuu wa Idara ya Mawasiliano kutoka NMB, Bw. Vicent Mnyanyika amesema, kwa mwaka huu wa 2022 benki ya NMB kupitia mbizo za hisani (NMB Marathon) imepanga kutimiza lengo la makusanyo ya shilingi Bilioni moja kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye tatizo la Fistula kupitia taasisi ya CCBRT  huku akisema lengo hilo ni mwendelezo wa adhma iliyowekwa tangu misimu wa kwanza mwaka 2021 uliofanikisha makusanyo ya shilingi milioni 400, huku wakitegemea kumaliza kiasi kilichobaki kwa msimu huu wa pili kwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 600.

Bw, Vicent aliongeza kwamba, walichagua kutatua tatizo la fistula kwani limekuwa ni changamoto kubwa sana kwa wanawake na wakina mama huku gharama ya matibabu kwa tatizo hilo ikiwa ni ya gharama na ya juu sana. Bw. Vicent aliongezea kwamba, wamejumuika na EFM na TVE  kwa sababu waliona ni vyombo vya habari pekee ambavyo vinaweza kutimiza adhima yao, na kuhakikisha shilingi milioni 600 zinakusanywa ndani ya msimu wa pili wa NMB Marathon kwa kutumia nguvu ya vyombo hivi vya habari ilivyo navyo.

Nae Bw, Mlang’a David Marealle ambaye ndie Meneja wa Mbio za hisani za NMB Marathon, alitoa wito kwa wananchi wote wa Tanzania na wadau mbalimbali kujiandikisha kupitia tovuti ya (marathon.nmbbank.co.tz) huku pia akitaja vituo tofauti tofauti ikiwemo Juliana na Mlimani City ambapo watu wanaweza kujiandikisha kwa siku za Ijumaa mpaka Jumapili huku akielezea gharama za usajili ni shilingi 20,000 kwa mbio za kilomita 5 na kilomita 10, huku mbio za kilomita 21 zikiwa ni shilingi 30,000.

Mkurugenzi wa ufundi NMB Marathon ambae pia ni mshindi wa zamani wa medali ya fedha ya michuano ya Olimpiki, Suleimani Nyambui ameelezea kwamba amefurahishwa sana na ushirika wa EFM na TVE kwenye NMB Marathon kwani anaamini wana uzoefu mzuri katika kutoa hamasa ya michezo huku akihusianisha uwepo wa EFM jogging club kwenye taasisi ambao ndio wahamasishaji wakuu wa mbio za pole nchini Tanzania na hivyo kuamini mchango mkubwa utakaotolewa na EFM na TVE katika kuhamasisha mbio za hisani za NMB Marathon kwa msimu wa pili. Bw Nyambui ameelezea namna mbio hizo zitakavyokuwa kimandhari pamoja na kuahidi wadau watakao jitokeza kufurahia mbio hizo kwa kupata nafasi ya kuona vivutio mbalimbali vya jiji la Dar es salaam ikiwemo Tanzanite Bridge lakini na uwepo wa vituo vya kutosha vitakavyogawa maji yaani (water points) kwa wakimbiaji.

Nae mkurugenzi wa uendeshaji kutoka EFM na TVE Ndugu Denis Busulwa (Ssebo) alielezea furaha ya EFM na TVE kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuinua masuala ya kijamii huku akiamini ushirika wa EFM Na NBM ni ushirika mkubwa unaokutanisha uthamani (Brand) wa taasisi zote mbili katika kunyanyua masuala muhimu ya kijamii ikiweno afya. Alieleza kwamba EFM inapenda kuchukua marathon hii kama kipimo kwa taasisi ya EFM kuonyesha ukubwa wake kwani ni muda mfupi utakaotumika kuitangaza huku akitegemea matokeo makubwa ikiwemo muitikio wa watu wengi kujisajili na kushiriki mbio hizo za hisani. Nae alimalizia kwa kuwakaribisha wananchi wote kushiriki mbio hizo na kusema kwamba “nmb marathon itakuwa ya utofauti sana, kwanza itahusisha pre-party itakayo fanyika kwa masaa yasiyopungua 20, na baada ya hapo washiriki wote waliojisajili watapata nafasi ya kupata supu kwa pamoja kasha kuchukuliwa na bus litakalowapeleka mpaka uwanjani”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents