Michezo

Nusu fainali ya FC Monaco Vs Juventus kupigwa leo

Mashabiki wa soka watashuhudia nusu fainali ya pili leo, baada ya nusu fainali ya kwanza kupigwa hapo jana.
Usiku wa leo itachezwa mechi kati ya klabu ya FC Monaco dhidi ya Klabu ya Juventus, huko Stade Louis jijini Monaco.

Mshambuliaji wa kikosi hiko cha FC Monaco, Radamel Falcao amesema hana mpango wowote wa kuondoka katika klabu hiyo ambayo inafukuzia mataji mawili msimu huu, Ubingwa wa League 1 na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika nusu fainali ya kwanza, mshambuliaji wa klabu ya soka ya Real Madrid, Christiano Ronaldo, ameonekana kua mwiba mchungu baada ya kuiwezesha timu yake ya Real Madrid kuichapa Atletico Madrid mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza uliopigwa hapo jana katika dimba la Estadio Santiago Bernabeu jijini Madrid.

Ronaldo alipachika mabao hayo katika dakika ya 10 kipindi cha kwanza na kuandika bao la pili dakika ya 73 kipindi cha pili ,huku akihitimisha karamu ya mabao matatu dakika ya 86 kipindi cha pili.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents