Burudani

Pam D awataja wasanii anaotamani kuwashirikisha

Pam D ni mmoja wa wasanii wapya wa kike wanaofanya vizuri kwa sasa.

pamd

Uwezo wake ulionekana kwenye wimbo ‘Nimempata’ aliomshirikisha Mesen Selekta. Ameimbia Bongo5 kuwa kazi yake mpya itatoka hivi karibuni na kwamba Mr Blue na Juma Nature ndio wasanii anaowakubali na angependa kufanya nao kazi.

“Unajua tokea nakua, wasanii ambao nilikuwa natamani kufanya nao kazi ni Mr Blue na Juma Nature maana ni wasanii ambao wanapendwa sana hata wasipotoa ngoma. Lakini wakipanda katika jukwaa lolote unaona wanavyopokelewa. Juma Nature tumeshaongea tayari kwahiyo muda wowote nitafanya naye kazi. Mr Blue bado sijaongea naye. Kwa upande wa wasanii wa kike kwakweli natamani sana kufanya kazi na Vanessa Mdee, namkubali sana.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents