Burudani

Peter Msechu atoa kali nyingine, ni kuchapwa fimbo 6 hadharani

Msanii wa Bongo Flava, Peter Msechu ametoboa siri ya kuwahi kushika nafasi ya mwisho darasani katika mtihani wa hesabu kipindi akisoma kidato cha tano na sita (advance level) kitu kilichopelekea kuchapwa fimbo 6 hadharani .

kupitia ukurasa wake wa Instagram amebainisha hayo na kueleza kuwa kitendo hicho kilimfedhehesha sana kwa kuwa kilitokea mbele ya wadogo zake (O Level).

Mchana wa leo Tanga Nilipotembelea shule niliyosomea advance level GALANOS SEC SCHOOL.

Hapa niliposimama ndio sehemu ya assembly Kuu Kila jumatatu Hii ndio sehemu jumatatu moja hivi mbele ya wanafunzi wote wa O level na A level nilitangazwa wa mwisho katika mtihani wa darasani wa hesabu(pure mathematics) kuwa Mimi ndiye nimeshika nafasi ya mwisho, nilitangazwa baada ya headmaster kusikia wanatangazwa walioongoza katika mtuhani huo wakipewa Zawadi. Baada ya yeye kusikia hivyo kwa lengo la kutaka kuonyesha hataki Watu wafeli Shuleni kwake akaagiza aliyeshika mkia katika mtihani huo aje mbele naye apewa Zawadi yake (KUCHAPWA FIMBO 6 HADHARANI).

Siku hii niliumia Sana sana kwani niliona Kama nimedhalilishwa Sana pale Shuleni kitendo cha mm kutambulishwa wadogo zangu O level na shule nzima kiujumla kuwa nimekuwa wa mwisho.

Siwezi laumu kwani huwenda wao walihisi ni njia sahihi kwa Kipindi kile kunisaidia. Ila ninachokumbuka matokeo yake baada ya ile hali kutokea wanafunzi wa O level hawakuniheshimu tena hata walipokuja Kwenye Darasa letu la A level(EGM) kuja kuuliza maswali hakuna aliyeniuliza kwani waliona SINA AKILI na siwezi msaidia.

Ilinisumbuaga Sana kwa muda mrefu Ila kwa sababu nilikuwaga waruwaru nilikuja kuzoea baadae ila tokea Siku hiyo kwangu naamini ilikuwa Siku ya mwisho kutamani kuipenda shule. Nilirudi nyuma Sana Sana na nikawa kilaza Namba moja darasani nisiyejiweza.

LEO HII NINAJIFUNZA JAMBO KUWA MUNGU NDIO HUPANGA HATIMA YA MTU NA SI MWANADAMU. LEO HII NAKUJA HAPA NATAFAKARI SANA KWANINI MUNGU ASIITWE MUNGU?? #KAZANAnaUNACHOKIAMINI

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake itwayo Yakawa baada ya kubamba na ngoma ‘Nasema Nawe’ aliyoshirikishwa na Tabla.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents