Burudani

Phil Collins kufunga ndoa tena na mke wake baada ya kupeana talaka mwaka 2008!

Muimbaji wa Uingereza, Phil Collins amerudiana na mke wake na wanatarajia kuoana tena.

SCCZEN_300116APPC04032001801_620x310

“Kuachana kwetu ulikuwa ni uamuzi mbaya,” Orianne Collins, aliyeachana na staa huyo, aliiambia SonntagsBlick weekly. “Ninamuita Phil mume wangu tena.
“Tupo karibu mno kiasi ambacho haina tofauti kama tumeoana ama lah, lakini tumepanga kuoana kwa mara ya pili.”

Wawili hao waolifunga ndoa nchini Switzerland mwaka 1999, wana watoto wawili na walitengana mwaka 2006 na kupeana talaka miaka miwili baadaye. Hiyo ilikuwa ni ndoa ya tatu ya Collins, mwenye miaka 64, mwenye watoto watatu wengine kwenye ndoa zake za mwanzo.

Baada ya kupeana talaka, Orianne aliolewa na mwanaume mwingine waliyezaa naye mtoto mmoja.Hiyo ilikuwa sababu ya Phil Collins kujikuta akiwa mlevi lakini aliacha baada ya kuifuata familia yake jijini Miami.

Orianne, anayedaiwa kuachana na mume wake, amedai kuwa hajawahi kuacha kumpenda Collins. Amedai kugundua kuwa Collins ndiye mwanaume wa maisha yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents