Burudani

Picha: Ujenzi wa Show Room ya magari Kigamboni wafikia patamu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda  ametembelea na kukagua Maendeleo ya ujenzi wa miundombinu kwaajili ya ShowRoom zote za magari kwenye eneo Maalumu lililotengwa Kigamboni.

RC ameongozana na viongozi wa Taasisi mbalimbali ikiwemo TRA, SUMATRA, NSSF, Bank ya watu wa Zanzibar pamoja na Jeshi la Polis na Jeshi la Zimamoto na uokoaji ambao wameenda kuonyeshwa maeneo yaliyotengwa kwaajili ya Ujenzi wa Ofisi.

RC MAKONDA amesema kuwa lengo kuhamishia Showroom Kigamboni ni kufanya Kigamboni kuwa soko la Magari Africa, kuwapa Wananchi fursa ya kuchagua gari analotaka kwenye eneo moja, kuiwezesha Serikali kupata mapato na kupunguza wizi wa magari.

Akiwa kwenye eneo hilo ameshuhudia ujenzi wa miundombinu ya Barabara, Madaraja, Umeme na Maji ikienda kwa kasi kubwa.

Tayari baadhi ya Taasisi na wenye Showroom waliokabidhiwa maeneo wameanza kujenga ili kuhakikisha ifikapo January Mosi wanakuwa wamehamisha Showroom zao.

Ndani ya eneo hilo kutakuwa na ofisi za Taasisi zote zinazohusiana na biashara ya Magari ikiwemo TRA, TPA, SUMATRA, Bank, NSSF,Bima, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na uokoaji, Garage, Sheli na Wauzaji wa Vipuri vya Magari.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akipokea maelezo kutoka kwa wasimamizi wa biashara hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents