Habari

Prof. Makame amteua mwenyekiti wa bodi ya ushauri wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb), kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho yake kupitia Sheria Na. 13 ya mwaka 2009 amemteua Dkt. Edward Wilson Ngwale kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10.04.2017.

Mhe. Prof. Mbarawa amemteua Dkt. Ngwale kushika nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi baada ya uteuzi wa awali kufika ukomo.

Pamoja na uteuzi huo Profesa Mbarawa amewateua Wajumbe watano (5) wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania ambapo John Bura – Mkandarasi kupitia Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Pius P. Tesha – Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bakari M. M. Mwinyiwiwa – Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Ntuli Lutengano Mwakahesya – Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Amiri N. Mcharo – Wizara ya Fedha na Mipango

Imetolewa na;

Eng. Joseph M. Nyamhanga

KATIBU MKUU (UJENZI)

12.04.2017

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents