Habari

Profesa Lipumba aeleza sababu za ukaribu wake na serikali

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameleeza sababu za kuonekana mara kwa mara katika shughuli za kiserikali huku akidai kuwa haajanza juzi kuhudhuria shughuli hizo.

Profesa Lipumba ameeleza hayo alipokuwa katika kipindi cha Funguka kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Azam TV akiwa na mtangazaji, Tido Mhando. Akijibu swali hilo Profesa Lipumba alisema, “Kama nimealikwa katika shughuli ambayo Rais anafungua miundombinu yenye manufaa kwa taifa zima, siwezi kuacha kwenda. Nitahudhuria, nitakwenda tu kwa sababu maendeleo hayana chama.”

“Sijaanza juzi kuhudhuria shughuli za kiserikali, ukifuatilia utagundua kuwa huo ni utamaduni wangu tangu zamani. Nikialikwa katika shughuli za kiserikali na nikiwa na nafasi nimekuwa nikihudhuria,” aliongeza.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents