Habari

Video: RAHCO kula sahani moja na madalali tapeli

Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli Tanzania (RAHCO), imetoa onyo kali kwa wanaojifanya madalali wa kampuni hiyo ambao wamekuwa wakiwadanganya wakandarasi kuwa wanaweza kuwaunganisha kufanya kazi katika ujenzi wa reli ya kisasa.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO, Masanja Kadogosa wakati akitoa maendeleo ya mradi huo tangu uzinduliwe na Rais Magufuli.

“Hakuna kampuni au mtu yoyote ambaye ametumwa na Rahco kutafuta wakandarasi kazi zinatakiwa zipatikane kwa uwazi, kwanza anayeomba kazi anatakiwa aone ni kazi gani na ajue masharti ya kupata kazi hiyo upo utaratibu na sio kama unaofanywa a watu hao,” alisema Bw Kadogosa.

“Wapo watu wa aina hii wanachukua wasifu binafsi wa muomba kazi (CV) na fedha kwa kutumia jina letu, hatujatuma mtu yoyote kututafutia wafanyakazi wanapita na kuchukua fedha watu hawa ni wahalifu wanatakiwa kuchukuliwa hatua tumesharipoti kwenye vyombo vya sheria na wanafuatilia,” aliongeza Kadogosa

Video:

Hata hivyo alisema kudhibiti matukio hayo wana mpango na kampuni zinazotekeleza mradi huo kuanzisha tovuti ambayo itakuwa na nafasi hizo za kazi na taratibu za uombaji.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents