Habari

Raia wa Ulaya wapigwa marufuku kuingia Marekani (+Video)

Rais wa Marekani Donald Trump, ametangaza kuweka zuio kwa raia wa nchi za Ulaya kuingia nchini Marekani ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

Katika hotuba yake kwa njia ya Televisheni siku ya Jumatano, amesema safari zote za kutoka Ulaya zitazuiwa kwa siku 30 zijazo.

Lakini amesema ”hatua kali lakini zilizo na umuhimu” hazitaihusisha Uingereza, ambayo ina visa 460 vya virusi vilivyothibitishwa.

Kuna visa 1,135 vilivyothibitishwa nchini Marekani na watu 38 wameripotiwa kupoteza maisha.

”Kuzuia visa vipya kuingia Marekani, tutaahirisha safari zote kutoka Ulaya,” Trump alieleza.

”Hatua hii itaanza kutekelezwa kuanzia usiku wa siku ya Ijumaa”. Aliongeza.

Tump amesema Umoja wa Ulaya ”umeshindwa kuchukua hatua za tahadhari kama hizo” zilizoanzishwa na Marekani.

Unaweza pia kusoma

Alizungumza saa kadhaa baada ya Italia – nchi iliyoathirika zaidi baada ya China- kutangaza kuchukua hatua kali. Itafunga maduka yote isipokuwa yanayouza vyakula na dawa kama sehemu ya kujitenga.

Trump amesema kuahirishwa kwa safari pia kutahusu ”biashara na usafirishaji wa mizigo” kutoka Ulaya kuingia Marekani.

Pia ametangaza kutoa mkopo wa mabilioni ya dola kwa wafanyabiashara wadogo, na kutaka bunge la Congress kupitisha nafuu ya kodi ili kukabiliana na athari za mlipuko wa corona kiuchumi.

Hali ilivyo Marekani

Maafisa wamesema hatari ya maambukizi ilikuwa chini, lakini hali ilibadilika baada ya ongezeko la idadi ya visa vipya vya maambukizi vilivyothibitishwa mwanzoni mwa mwezi Machi.

Jitihada za kudhibiti zimeanza. Vikosi vimepelekwa kwenye mji wa New Rochelle, ulio kaskazini mwa New York, ambapo mlipuko huo unaaminika kuanzia huko.

Vikosi vya ulinzi vitatoa chakula kwa baadhi ya watu ambao wametakiwa kujiweka karantini.

Gavana wa jimbo la Washington amepiga marufuku mikusanyiko katika kaunti kadhaa. Jimbo lililo Kaskazini Magharibi ni kiini cha maambukizi nchini Marekani, kukiwa na idadi ya vifo 24 kati ya 38 nchi nzima.Mkuu Shirika la Afya Duninai (WHO), Dkt Tedros Adhanom Ghebreyes usametangaza mlipuko wa Corona kuwa janga la kimataifa

Mkuu Shirika la Afya Duninai (WHO), Dkt Tedros Adhanom Ghebreyes usametangaza mlipuko wa Corona kuwa janga la kimataifa

Hali ilivyo duniani

Shirika la Afya duniani limeutangaza mlipuko wa virusi vya corona kuwa ni janga la kimataifa, huku mlipuko huo ukiendelea kusambaa katika mataifa mbalimbali duniani.

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kuwa idadi ya visa nje ya China vimeongezeka mara 13 kwa kipindi cha majuma mawili yaliyopita.

Amesema kuwa “anahofu kubwa ” kutokana na “viwango vya maambukizi ” ya virusi.

Janga ni ugonjwa ambao unasambaa katika nchi nyingi kote duniani kwa wakati mmoja.

Italia

Waziri Mkuu Giuseppe Conte alitangaza ongezeko la masharti ya kujiweka karantini kuongezeka.

Alisema maduka mengi, migahawa, saluni, vitafungwa mpaka tarehe 25 mwezi Machi.

Italia ina watu 12,000 waliothibitika kuambukizwa na idadi ya waliopoteza maisha ni 827. Karibu watu 900 wenye maambukizi wako kwenye hali mbaya, WHO imesema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents