Habari

Rais Kikwete akamata #10 katika orodha ya viongozi wanaofanya vizuri Afrika, Rais wa Mali aongoza

Rais Jakaya Kikwete, amekamata nafasi ya 10 katika orodha ya viongozi wa nchi za Afrika zilizo chini ya jangwa la Sahara kwa mujibu wa survey iliyofanywa na kampuni ya maoni ya Gallup.

Jakaya Kikwete

Nafasi ya kwanza imekamatwa na Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita na kufuatiwa na Ian Kahama wa Botswana. Nafasi ya tatu imekamatwa na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta akifuatiwa na Rais wa Cameroon, Paul Biya.

Naye Yoweri Museveni wa Uganda ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 27 amekamata nafasi ya 9. Robert Mugabe wa Zimbabwe ambaye amekuwa madarakani kwa 26 amekamata nafasi ya 21 wakati Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo akikamata nafasi ya 24.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents