Habari

Rais Magufuli aitaka Israel kufungua ofisi ya ubalozi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli ametoa wito kwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kufungua ubalozi wa Israel hapa nchini.

Rais Magufuli alisema hayo Alhamisi hii alipokutana na balozi wa Israel hapa nchini, Yahel Vilan Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais alimhakikishia balozi huyo kuwa Tanzania imedhamiria kuimarisha na kukuza uhusiano na ushirikiano wake na taifa hilo.

Katika taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasilino ya Rais, Ikulu, Rais Magufuli amesema ili kufanikisha dhamira hiyo Tanzania imefungua ubalozi nchini Israel na amemuomba balozi huyo kupeleka ujumbe kwa Netanyau kuhusu nchi hiyo kufungua ofisi za ubalozi nchini.

Rais Magufuli amemuhakikishia kuwa Tanzania imedhamiria kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake na Israel hususani kwenye masuala ya uwekezaji, biashara, utalii na uboreshaji wa huduma za jamii.

Aidha Rais Magufuli alisema ili kufanikisha dhamira hiyo Tanzania imefungua Ubalozi Isarael na amemuomba Mhe Yahel Vilan kupeleka ujumbe kwa waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuwa Tanzania itafurahi kuona Israel inafungua ubalozi wake hapa nchini.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents