Habari

Rais Magufuli akutana na mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William, waongea kiswahili (+video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Septemba 27, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William aliyeambatana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke pamoja na ujumbe wake mara baada ya kuwasili hapa Nchini.

Wengine waliohudhuria mazungumzo hayo ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla akiwa pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa. Palamagamba Kabudi.

Prince Wiliam yupo nchini tangu jana akiwa ktk ziara ya siku 3 inayoangazia juhudi zinazofanywa na serikali ya Tanzania katika kukabiliana na ujangili

Katika hali ya kushangaza mjukuu huyo wa Malkia amezungumza na kusalimia na Rais Magufuli kwa lugha ya kiswahili. Tazama video.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents