Habari

Rais Magufuli amtumbua mtumishi aliyechana kitabu cha Quran ”Mimi namfukuza moja kwa moja” (+Video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemfukuza kazi Mtumishi wa Halmashauri ya Kilosa, Morogoro Daniel Maleki miaka 30 ambaye ni Afisa wa Kitengo cha Biashara ambaye alionekana kwenye video fupi akichana Kitabu cha Quran.

Rais Magufuli amemfukuza mtumishi huyo hii leo tarehe 11, Febuari, 2020 wakati akizindua Jengo la Manispaa ya Kigamboni na Jengo la Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni katika Eneo la Gezaulole Kigamboni Jijini Dsm.

”Juzi nilikuwa namsikia Mhe. Jafo, mtu mmoja kule Kilosa nafikiri alichana Kitabu kitakatifu, nakushukuru umechukua hatua ya kumsimamisha kazi. Lakini mimi namfukuza moja kwa moja, muandikie barua ya kuondoka moja kwa moja. Ashinde kesi asishinde huyo sio mfanyakazi wa Serikali. Hatuwezi tukakaa na wafanyakazi wapumbavu katika serikali hii, umechukua jukumu lako la kumsimamisha kazi, mimi namfukuza.” Amesema Rais Magufuli

Ujumbe wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo alipogiza kusimamishwa kazi kwa Mtumishi wa Halmashauri ya Kilosa, Morogoro Daniel Maleki miaka 30 ambaye ni Afisa wa Kitengo cha Biashara akionekana kwenye video fupi akichana kitabu cha Quran tukufu ambacho hutumiwa na Waislamu.

https://www.instagram.com/p/B8RX87KhZrz/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents