Habari

Rais Magufuli aongoza kikao cha Kamati Kuu ya chama cha CCM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Dkt John Pombe Magufuli ameongoza kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho kilichoanza leo Jumatano ya Sept 26,2017 Ikulu Jijini Dar Es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli akiwasili ukumbini kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Sept 27, 2017 Ikulu Jijini Dar Es Salaam


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Ndg. Phili Mangula akikaribishwa ukumbini katika kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho kilichoanza leo Jumatano ya Sept 27, 2017 Ikulu Jijini Dar Es Salaam.



Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Sept 27, 2017 Ikulu Jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na nyuma ya Makamu wa Rais ni Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa na Spika wa Baraza wa Wakilishi la Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichoanza leo Jumatano ya Sept 27, 2017 Ikulu Jijini Dar Es Salaam.

Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wote wa Halmashauri Kuu,wakiwemo Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Alli Mohamed Shein,Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Alli Idd.

PICHA NA IKULU.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents