Habari

Rais Magufuli apokea taarifa kutoka SADC, China na EU Ikulu Dar (Picha)

Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Stergomena Tax, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Manfred Fanti na Balozi wa China nchini, Wang Ke, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa SADC amesema Dkt. Stergomena Tax amefika Ikulu kutoa taarifa ya utekelezaji wa masuala mbalimbali ya SADC ikiwemo uendelezaji wa viwanda na kanda huru ya biashara ambapo wamekubaliana kuendelea kuhamasisha nchi wanachama kuendeleza viwanda ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi.

Aidha kwa upande wake Balozi wa Umoja was Ulaya (EU) nchini, Manfred Fanti amesema mazungumzo yake na Rais Magufuli yamekuwa na manufaa ambapo wamejadili namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na EU na kwamba tayari wameshakamilisha mazungumzo yaliyoruhusu kuendelea kwa mpango wa EU kuchangia bajeti ya maendeleo ya Tanzania ambapo shilingi Bilioni 132 zilizokuwa zimezuiwa sasa zimeruhusiwa na wanaandaa mpango mwingine wa miaka saba (7) utakaoanza mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents