Habari

Rais Magufuli atoa maagizo mazito kwa Kamishna Uhamiaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka Idara ya Uhamiaji kuendelea kushughulikia wahamiaji haramu  pasipo kumwogopa mtu yeyote yule.

Rais Magufuli amezungumza hayo leo, wakati  akizindua Hati ya kusafiria ya kielektroniki jijini Dar es Salaam, ambapo ameipongeza wizara ya Mambo ya Ndani.

“Wizara ya Mambo ya Ndani nawapongeza sana, waziri wa Mambo ya Ndani baada ya kulijua hili kwasababu nilipomteua kupeleka pale nikamwambia kuna mchezo mchafu unachezwa pale  ndio bongo land na wizara ya Mambo ya Ndani ina changamoto nyingi sasa immagration mmezitatua hizo changamoto asanteni sana,“ amesema Rais Magufuli.

“Na ndio maana kamishna wa migration alivyoniambia kuwa wanahiotaji nyumba  za wafanya kazi wa migration Dodoma sijatoa kwa taasisi nyingine nyumba lakini nilitoa hela serikalini tukatoa nyumba 103  kule Dodoma  ni kwasababu ya uzalendo ambao nimeanza kuuona na leo na kwamba hamjaniomba lakini pia mimi nimejiandaa kuja kutoa hela nyingine Makao Makuu mmeshakubali kuhamia Dodoma  na hapa palivyokaa kaa hapa hapakai kama makao makuu ya imagration, ninajua kuna baadhi ya wafanyakazi watalaumu kuhamia Dodoma.“

“Lakini ni lazima tuwe na jengo zuri  ambalo limekaa kweli kama  Makao Makuu ya Imagration lina packing nzuri kwahiyo Dkt. Makakala  katafute eneo  nitawapa  Bilioni 10 wakati wowote mtakapo zihitaji muanze kujenga Makao makuu na ninatoa hivi kwa shukurani unayofanya wewe pamoja na watendaji wako  endeleeni kuchapa kazi, endeleeni kubadilisha jina la uhamiaji endeleeni kushughulikia wahamiaji haramu  bila kujali bila kumuogopa mtu yoyote,“ ameongeza Rais Magufuli.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents