Habari

Rais Magufuli kuna siku nilikuandikia ushauri, ukaniambia ni mbovu – Mzee Makamba

Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Yusuph Makamba amemmwagia sifa, Mwenyekiti mpya wa chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwa muwazi kwa kila jambo huku akitolea mfano kuwa kuna siku alimuandikia ushauri na kiongozi huyo alimjibu na kumuambia ushauri huo mbovu.

Akiongea katika Mkutano Mkuu wa 9 wa CCM alipopewa nafasi ya kuzungumza amesema kuwa kazi yao kubwa waliotangulia ni kuwashauri waliopo madarakani.

“Rais Magufuli hivyo ulivyo asali hauilambi kwa aibu kuna siku moja nilikuandikia ushauri ukaniambia ushauri mbovu siutaki hivyo ndivyo inavyotakiwa maana moja ya kazi yetu sisi tuliopumzika ni kuwa shauri nyinyi mliopo kama mshauri ni mbovu unasema asante mzee Makamba ushauri huu mbovu mimi nilipenda siku kasirika,” alisema Mzee Makamba.

“Chama hichi kinafaa kuongozwa na watu amkaini kama wewe huna majivuno, huna makuu bwana Mtume alisema ukimsifu mtu mwenyewe wakati yupo una mtukana ila mimi nakusifu na sina maana ya kukutukana.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents