Habari

Rais Museveni apiga marufuku makampuni ya kubashiri na kubeti nchini Uganda

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ametangaza rasmi kuyafutilia mbali makampuni ya michezo ya kubashiri na kubeti nchini humo.

Image result for museveni bans betting

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Fedha nchini humo, 
David Bahati amesema Rais Museveni pia amekataza kutoa leseni za usajili kwa makampuni hayo.

Wizara imepokea maagizo kutoka kwa Rais akitaka makampuni yote ya kubet na kubashiri kufungwa mara moja. Pia katika maagizo yake ametaka Wizara isitishe kutoa leseni za usajili kwa makampuni ya aina hiyo, na tayari Wizara imefanya mawasiliano na bodi ya Michezo ya Kubashiri“amesema David Bahati kwenye hotuba yake fupi katika kanisa la 
Brethren, Dayosisi ya Kigezi Jumapili iliyopita .

Hata hivyo, Bodi ya michezo ya kubashiri nchini humo, kupitia kwa Mwenyekiti wake, Manzi Tumubweine amesema kuwa amepata taarifa hizo lakini hajapokea barua rasmi kutoka serikalini.

Kwa kufuta makampuni hayo, Uganda itapoteza Shilingi Bilioni 50 kwa mwaka .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents