Uncategorized

Huu ndiyo ujumbe wa mwisho wa Emiliano Sala kabla ya kupotea angani na ndege ‘Nimejawa hofu, ndege inaelekea kuanguka’

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Cardiff City aliyeweka rekodi ya usajili ndani ya timu hiyo, Emiliano Sala alipata nafasi ya kutuma ujumbe mfupi wa sauti ndani ya ndege kwa baadhi ya ndugu na marafiki zake kupitia mtandao wa ‘WhatsApp’ unaotaka kumtafuta kama watakosa habari zake ndani ya saa moja na nusu.

Straika huyo wa Argentina alisainiwa siku ya Jumamosi akitokea klabu ya Ufaransa ya Nantes kwa dau la pauni milioni 15 na kupanda ndege kuelekea Cardiff kabla ya kupotea kwenye rada mara baada ya kufika umbali wa maili 12 kutoka Kaskazini mwa Kisiwa cha Guernsey siku ya Jumatatu.

“Nipo ndani ya ndege muda huu naelekea Cardiff, kesho nitaanza mazoezi na timu yangu mpya. Lakini inaonekana kama ndege itaanguka,” alisema Sala kupitia ujumbe wa sauti aliyoutuma kwa marafiki zake kupitia mtandao wa WhatsApp.

Sala ameongeza ”Kama hutopata habari zangu zozote ndani ya saa moja na nusu sioni kama kunasababu ya kumtuma mtu wa kunitafuta, nimejawa na hofu.”

Bado shukhuli za utafutaji zinaendelea tena hii leo kupitia, Helicopters na Boti za uokoaji kwenye kisiwa hicho cha Guernsey baada ya kusitishwa usiku wa jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents