Burudani

Rapper Witness awachana waongozaji wa video wa Bongo

Rapper wa kike, Witness amewachana waongozaji wa video wa Tanzania anaowashutumu kwa ubabaishaji.

Joson-Gete-na-Witness

“Leo kwa sababu ni bday yangu nitapenda kusema ukweli juu ya kitu kimoja,” aliandika jana kwenye ukurasa wake wa Facebook.

“Mbali na sababu za kibiashara ya kuwa artists wengi wameamua kuwa wanaenda kushut video zao za muziki nje ya nchi na kugharamia fedha nyingi tofauti na ndani moja huwa video zinatoka on time,mbali na hayo huwa wenzetu wanajiongeza kwa kusambaza wenyewe especially kwenye tv stations za nje amazon ni ndoto ya kila msanii video zake kuchezwa huko, sasa bas turudi hapa Nymbani utakuta mtu anataka sana mfanye kazi na kwa wakati huo huo unakua umempa ratiba video yako unataka itoke lini anatokea kukaa nayo miezi miwili hadi mitatu jamani kweli hii ni haki wakati na wewe unategemea video ndo ufanye bishara?,” alihoji.

“Je huku siyo kurudishana nyuma jamanii? Ama ndo tunadumisha usemi usemao sisi ni makalio ya dunia? Hili suala huwa linaniudhi sana na mtu kama huyu akiona unampigia sana Anazima na simu kabisaa Wenye makampuni ya video acheni kabisa hii tabia inashusha sana hali ya uchumi,hadhi,inakera na inaonesha ni kiasi gani msivyo proffessionals na hamna ueledi upendo na ufanisi katika kazi zenu, ninatumai mtajirekebisha kila mtu kwa wakati wake.”

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents