Habari

RC Ruvuma, Christina Mndeme ataka kuzingatiwa kwa usalama na afya kwa wamiliki wa viwanda (+Video)

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewataka wamiliki wa viwanda mkoani Ruvuma kuzingatia usalama na afya katika maeneo yao ya kazi.


Akizungumza katika uzinduzi wa maonyesho ya viwanda mkoani Ruvuma, Mndeme amesema wanapozalisha bidhaa mbalimbali lazima wazingatie swala zima la usalama ili kuepukana na majanga ambayo yanaweza kutokea na hivyo kusisitiza elimu ya usalama na afya mahala pakazi kuzingatiwa.

Kwa upande wake mtaalamu wa mazingira kutoka wakala wausalama na afya mahali pakazi (OSHA) JOSSAM KAMANZA amese ili kufikia malengo na kuimalisha usalama katika mahala pakazi lazima kuwepo na ushirikiano baina ya mwajiri na mwajiliwa.

Maonyesho ya viwanda mkoani Ruvuma yamezinduliwa leo katika kiwanja cha maji maji mjini songea na mkuu wa mkoa huo Cristina Mndeme na kilele kitakuwa tarehe 26/07/2019/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents