Burudani

RECAP: Wasanii wa Tanzania watumie mabifu yao kifursa kama Ruger na Bnxn (Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO amezungumzia namna Ruger na Buju kutoka Nigeria walivyomaliza bifu lao.

Amesema anashangaa wasanii wetu Tanzania wanamaliza bifu wanabaki wanapiga picha tu badala ya kuingia Studio na kutoa ngoma.

Amesema mfano mwingine wa kuigwa na TID na Q CHILLAH walivyomaliza tofauti zao na kuingia Studio na kutoa ngoma lakini pia kuridisha Band yao.

Kama inavyofahamika Ruger na Bnxn (inasomeka kama benson) wengi walikuwa wakimfahamu kwa jina la Buju walikaa kwenye bifu muda mrefu, bifu ambalo lilianzishwa na mashabiki twitter na mwishowe kuja kuwavaa wasanii kama tunavyoonaga mabifu ya wasanii wetu hapa Bongo mfano Diamond na Harmonize au Diamond na Alikiba.

Wawili hao waliamua kukaa chini na kuona waachane na maswala ya mabifu na kuamua kuungana kuachia project ya pamoja yan EP ambayo imetoka leo 18th April ikiwa na ngoma 7.

Ngoma ya kwanza ilitoka Romeo must die ilitoka February na tayar ina streams zaidi ya milioni 15 kwenye platforms zote, ngoma ya pili imetoka Last week April inaitwa POE hii unayoisikiliza na ina streams za kutosha tu

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

Host: @el_mando_tz Cameraman @samirkakaa

Kuangalia video kamili Bonyeza Link hapa chini:
https://youtu.be/66EJa3o5kLE?si=kpMApurU2pO5CyXd

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents