Burudani

Rich Mavoko kufanya collabo na rapper Rabbit wa Kenya

Ikiwa haijafikisha hata wiki tatu tangu video yake ya ‘Pacha Wangu’ itoke, Rich Mavoko ameanza kula matunda ya wimbo wake mpya huo.

IMG-20141009-WA0000

Msanii huyo anatarajia kufanya collabo kuwa na rapper wa Kenya, Rabbit aka Kaka Sungura. Kupitia akaunti yake ya Instagram, Mavoko ametease kava ya ngoma hiyo.

“Rabbit ni msanii mkubwa sana wa hiphop toka Kenya ambaye anaheshimika sana nchini mwao,” Mavoko ameiambia Bongo5. “Jamaa ni mfuatiliaji mzuri wa muziki wa Bongo na alifuatilia kwa ukaribu sana launch ya wimbo wangu wa Pacha Wangu online tuliouachia saa saba usiku. Kifupi mashabiki wangu Afrika Mashariki watarajie ngoma kubwa sana baina yangu na Kaka Sungura wa Kenya pamoja na vitu vingine vingii kutoka kwa Mavoko,” aliongeza.

Rabbit anafahamika kwa ngoma kali kama ‘Sitaki Kukuona’, ‘Tulia tu’aliomshirikisha rapper wa Afrika Kusini, HHP. Pia hivi karibuni aliwashirikisha Weusi kwenye ngoma yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents