Burudani

Rihanna ajitolea kuwalipia karo wanafunzi wasio jiweza

Msanii wa muziki Rihanna amejitolea kufadhili elimu ya wanafunzi kupitia wakfu wake.

7677_5U4Ffj1968-559x520

Hatua hiyo inaamanisha kwamba watu kutoka jamii zisizojiweza watapata msaada wa kulipa ada ya shule.

Wakfu huo wa Clara Lionel umekuwa ukifanya kazi tangu 2012 ambapo hutoa ruzuku kwa shule huko Barbados mbali na kuwasaidia wagonjwa wa saratani.

160512081605_clf
Hii Nembo ya wakfu wa Rihanna

Bibiye Rihana alifariki kutokana na ugonjwa wa saratani mwaka huo huo na hivyobasi kumfanya yeye kuanza kusaidia sekta ya matibabu.

Kwa sasa shirika hilo limepanuka na kutoa ufadhili wa elimu hadi kufikia dola 50,000 kwa wanafunzi waliopo Barbados,Brazil,Cuba,Haiti,Guyana,Jamaica na Marekani.

”Sidhani kwamba ni haki kwa watoto kubeba mzigo wa kifedha katika miaka walio nayo”,alisema Rihanna.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents