Michezo

Ripoti ya Gamondi yashtua Mabosi Yanga

Licha ya mazota yaliyopo ya ripoti za makocha kutolewa mwishoni mwa msimu kwa upande wa Yanga mambo ni tofauti baada ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi kuwasilisha mapema ripoti kwa Mabosi wa klabu hiyo ikiwa ni mikakati ya kuanza kukisuka upya kikosi chamsimu ujao.

Miguel Gamondi

Hesabu za Gamondi ambaye jioni ya jana alikuwa uwanjani kuiongoza timu hiyo dhidi ya Singida Fountain Gate katika mechi ya Ligi Kuu Bara ni kuhakikisha anakuwa na kikosi imara zaidi kuliko alichonacho sasa na tayari mabosi wa klabu hiyo wameanza kuipitia na kuifanyia kazi mapendekezo aliyoyatoa kwao mapema.

Gamondi

Mabosi wa Yanga kwa sasa akili zam zimegawanyika kuna upande unasimamia namna gani watamaliza mechi za Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho (FA) , lakini upande mwingine umeanza kuangalia namna ya maboresho zaidi ya kikosi hicho kutokana na mapendekezo ya Gamondi.

Utakapoongea na mabosi wa Yanga kuhusu zuio la usajili na shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) na lile la (Tanzania) watakujibu kwamba tutamalizana nao tu baada ya hapa wanaendelea na majukumu Yao kama kawaida.

Mabosi hao wameshapokea ripoti ya awali ya usajili kutoka kwa benchi la ufundi chini ya kocha huyo raia  wa Argentina inayotaka maskine mpya tano (5) kwa msimu ujao na kushtua kwa kubariki baadhi ya wachezaji kufyekwa.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni kwamba ripoti hiyo imeonyesha itahitaji kuongeza kipa mmoja atakayechukua moja ya nafasi ya makipa watatu waliopo sasa akiwemo Djigui Diarra, Metacha Mnata na Mshery mmoja kati ya hawa atapewa mkono wa kwaheri.

Kwenye ukuta hasa eneo la mabeki ripoti hiyo imeonyesha kuhitaji beki mmoja wa kushoto ambapo hapa kuna uwezekano mkubwa wa mkongwe Joyce Lomalisa akapewa mkono wa kwaheri kwani mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa zaidi zinasema kuwa kwa sasa Yanga bado inaendelea na mazungumzo na mabosi wa Singida Fountain Gate juu ya kurefusha mkataba wa Beki wa kushoto wa Nickson Kibabage anayetumikia Yanga kwa mkopo ambapo benchi la ufundi la Yanga limeonyesha mahitaji ya kuendelea naye.

Ripoti hiyo, inaelezwa pia inahitaji kiungo mkabaji mwenye ubora zaidi au sawa na Khalid Aucho atakayejiunga kikosini kuungana na Mganda huyo pamoja na Jonas Mkude aliyepindua meza Kibabe kwa kubakishwa baada ya kuonyesha kiwango kikubwa kwenye mechi mbili dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Gamondi pia inaelezwa anahitaji winga mmoja na mshambuliaji wa maana watakaokuja kuongeza nguvu kwenye eneo la mwisho ambalo bado mshambuliaji Joseph Guede ameanza Cheche akifunga jana dhidi ya Singida Fountain Gate.

Kwenye winga kuna Skudu Makudubela na Denis Nkane ambao wamekosa namba.

 

 

 

Chanzo; Mwanaspoti

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents