Rwanda kinara nchi 10 zinazoongoza kwa usafi Afrika

Nchi ambazo zina hewa safi zaidi haziwi kwenye hatari ya kuwa na mazalia ya wadudu ambao wanaweza kusabababisha magonjwa ambayo yana uhusiano na uchafuzi wa hali ya hewa kwa mfano magonjwa mbalimbali ya mfumo wa upumuaji au magonjwa ya moyo.

Nchi ambazo zina kiwango kikubwa cha uchafuzi wa hali ya hewa ziko hatarini zaidi kuwa na viwango vikubwa vya magonjwa yasiyokuambukizwa na kuchangia asilimia 72% ya vifo vyote, asilimia 16 katika vifo hivyo vinachangiwa na sumu inayotokana na uchafuzi wa hali ya hewa.

Watafiti kutoka Chuo kikuu cha Yale na Columbia wakishirikiana na World Economic Forum wamefanya tathimini ya usafi na mazingira kwa nchi zaidi ya 180 duniani.

Vigezo mbalimbali muhimu vinazingatiwa kupata orodha ya nchi safi duniani kwa mfano hewa safi (miji ama maeneo ya nchi kutokuwa na harufu mbaya), maji safi, usafi wa mazingira, bioanuwai, makazi ya watu na sera endelevu za kuhifadhi mazingira.

Kwa vigezo hivyo, zifuatazo ni nchi 10 zinazoongoza kwa usafi barani Afrika.

10. Namibia

Namibia

Ni nchi kutoka Kusini mwa Afrika. Viongozi wa nchi wamekuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za usafi wa mazingira, wakishiriki mara kwa mara katika mazoezi ya usafi. Mji wake mkuu, Windhoek ambao uliwahi kuwa jiji safi Afrika, kwa sasa linashika nafasi ya nne barani humo.

Nchi hiyo ina kampeni maalumu ya usafi wa mazingira iliyoanzishwa na kusimamiwa na Serikali, kampeni inayosaidia kuweka mazingira ya nchi hiyo katika hali ya usafi na kuwa na hewa safi. Pamoja na yote, lengo kubwa la kampeni hiyo ni kuongeza uelewa wa watu kuhusu masuala ya usafi na kanuni zake.

9. Botswana

Botswana

Botswana ilikuwa miongoni mwa nchi masikini zaidi duniani, lakini kwa jitihada za viongozi wake na sera zinazoeleweka zikasaidia nchi hiyo kupaa na kuwa moja ya nchi tajiri na zenye uchumi imara Afrika.

Pamoja na nchi hiyo kupambana kuwa nchi yenye uchumi imara, imepambana pia na kuwa moja ya nchi safi Afrika. Na ushahidi mzuri ni pale utakapowasili katika jiji la Gaborone, makao makuu ya nchi hiyo.

Mitaa ya jiji hilo ni misafi na imepangika vyema, foleni za magari sio ya kutisha kutokana na miundo mbinu mizuri ya barabara na kuna majengo ya vioo ya kisasa na yaliyobuniwa vyema.

8. Morocco

Morocco ilikuwa nchi iliyoongoza kwa usafi Afrika mwaka 2019, lakini imeshuka mwaka 2021 mpaka nafasi ya 8.

Morocco imeanguka mpaka nafasi hiyo kwa sababu kadhaa, lakini Serikali inaendelea kujaribu kuifanya nchi hiyo kuwa na maji safi, uwepo wa hewa safi na ushiriki wa wananchi wake kwenye masuala ya usafi.

Licha ya kudondoka mpaka nafasi ya 8 lakini jitihada za nchi hiyo za kuwa nchi iliyo juu kwa usafi zinaendelea, na haishangazi jiji lake la Ifrane kuchaguliwa kuwa jiji la pili duniani kwa usafi, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na NBC times, ambayo iliorodhesha majiji masafi 12 duniani.

7. Afrika Kusini

Africa Kusini

Afrika kusini ni moja ya mataifa yenye mvuto pamoja na maendeleo ya kuigwa Afrika. Lakini moja ya jambo ambalo nchi hiyo inalikazania wakati wote ni kuboresha suala la usafi licha ya idadi ya watu kuzidi kuongeza nchini humo.

Afrika Kusini ni nchi nzuri na safi, na baadhi ya majiji yake kama Cape Town, linatajwa kama jiji zuri linalovutia duniani. Afrika Kusini inashika nafasi ya 7 kwa usafi Afrika, ikishika nafasi ya 95 duniani.

6. Misri

Nafasi ya sita kwa nchi zinazoongoza kwa usafi Afrika ni Misri, moja ya nchi zinazotembelewa sana Afrika. Licha ya kuwa na idadi kubwa ya watu, Misri imefanikiwa kutunza usafi wa mazingira yake.

Maisha bora yaliyoko nchini humo, yanatajwa kama maisha mazuri kwa viwango vya Afrika, na watu wengi wanaoishi nchini humo wanaridhika na maisha yaliyoko. Ni nchi inayoshika nafasi ya 91 duniani ikiwa na miundo mbinu mizuri ya kuhifadhi taka, kudhibiti uchafuzi wa hewa na usimamizi mzuri wa rasilimali. Haishangazi kuwa miongoni mwa nchi zilizo na viwango vizuri wa usafi Afrika.

5. Algeria

Algeria, ni nchi kutoka Afrika ya Kaskazini ikiwa na fukwe nzuri za bahari ya Mediterania na sehemu ya jangwa maarufu la Afrika, jangwa la Sahara.

Kwa sasa nchi hiyo ina idadi ya watu wapatao 44.7 milioni kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2021. Algeria kwa muda mrefu imekuwa ikihaha kukabiliana na uchafuzi wa hali ya hewa.

Ikaanzisha sheria mbalimbali za kulinda na kuhifadha mazingira na mali asili.

Mapambano haya yameisaidia nchi hiyo kuwa miongoni mwa nchi zenye kusifika kwa usafi Afrika.

4. Mauritius

Mauritius

Mauritius iko nafasi ya nne kwa usafi Afrika na pia ni nchi yenye kuvutia watu wengi kwa vigezo kadhaa. Moja ni hati yake ya kusafiria ina nguvu ikishika nafasi ya pili duniani.

Ni miongoni mwa nchi zenye fukwe nzuri na za kuvutia Afrika lakini pia nchi nzuri kwa shughuli za kibiashara.

Pamoja na vitu hivyo vizuri, usafi ni kitu kinachofanya nchi hiyo kuwa na mvuto zaidi. Kwa sasa Mauritius inashika nafasi ya nne Afrika kwa usafi kulingana na utafiti ikishika nafasi ya 81 duniani.

Fukwe zaek nzuri na mitaa yake misafi itakufanya tu ukipende kisiwa hiki kinachopatikana katika bahari ya Hindi.

3. Gabon

Wengi wanaweza kupatwa na mshangao kuiona Gabon kwenye orodha hii, tena ikiwa miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri zaidi kwa usafi Afrika. Ukweli ni kwamba kwa miaka kadhaa Gabon imefanya kazi kubwa kushughulikia usafi na usafi wa mazingira kwa ujumla.

Licha ya kuwa miongoni mwa nchi zenye idadi ndogo ya watu, imekuwa moja ya nchi zinazotembelewa sana Afrika ya kati. Mwaka 2017 kupitia juhudi za pamoja za Shirika la afya duniani (WHO) na Shirila LA Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto (UNICEF), asilimia 90% maeneo ya mjini yana maji safi ya kunywa, lakini ni asilimia 49% pekee ya kaya zinapata huduma za msingi za usafi wa mazingira.

Katika maeneo mengi ya vijijini upatikanaji wa maji safi umeshuka kwa asilimia 55% huku huduma za msingi za usafi wa mazingira, zikishuka mpaka asilimia 37%.

2. Tunisia

Tunisia

Tunisia ni nchi ndogo ya Kiarabu kutoka Afrika Kaskaizni, ambayo inawakilisha mapambano ya dhati ya uhuru na vita dhidi ya ugaidi.

Pamoja na majirani zake Algeria na Libya, iko kusini mwa fukwe ya bahari ya mediterania.

Kwa miaka kenda na kenda eneo ilipo inawavutia watu wa jamiii mbalimbali, wazuri na wabaya wakiwemo magaidi. Lakini ikiwa na watu milioni 11.7 Morocco imekuwa ikipambana kuwa nchi yenye kutunza mazingira yake vyema na kusimamia usafio wa mazingira vyema.

Tunisia imeweka sera za kutosha za kusimamia kwa ufanisi masuala ya maji, nishati na uchafuzi wa hali ya hewa. Sera hizo kwa kiasi kikubwa zimeifanya nchi hiyo kushika nafasi ya pili Afrika kwa mwaka 2021, kwa nchi zenye mazingira safi na hewa safi Afrika. Duniani inashika nafasi ya 69.

1. Rwanda

Rwanda

Rais Paul Kagame wa Rwanda, anatambulika kwa namna anavyoweza kusimamia jambo lake, analolitaka, na eneo la usafi ni jambo alililopigania kwa muda mrefu. Ukiacha sifa zingine za kiusalama zinazoizunguka nchi hiyo kwa miaka kadhaa sasa nchi hiyo hasa jiji lake la Kigali, limekuwa miongoni mwa maeneo masafgi zaidi Afrika.

Rwanda imetajwa kuwa ni nchi yenye kuongoza kwa usafi Afrika kwa miaka mine mfulululizo.

Baada ya kukumbwa na vita na mauaji ya kimbari katika mwaka 1994 , imerejea na kuweka nguvu kwenye kujijenga na kjuwa nchi mfano sio tu Afrika bali duniani kwa ujumla.

Serikali ya Rwanda imekuwa ikichukua hatua kadhaa kuhakikisha suala la usafi wa mazingira linazingatiwa kwa mfano imepiga marufuku mifuko ya plastiki na kuanzisha kampeni maalumu za usafi wa mazingira.

Hatua hizi za serikali zimeifanya Rwanda kutajwa tena mwaka 2021 kama nchi inayoongoza kwa usafi barani Afrika.

Related Articles

Back to top button