Burudani

Saida Karoli atangaza ujio mpya (+Video)

Msanii mkongwe wa muziki wa asili, Saida Karoli ameweka bayani juu ya ujio wake mpya katika tamasha la muziki la Sauti za Busara kwa mwaka 2018.

Saida ambaye anatamba na vibao vyake matata ikiwemo, ‘Omulilo’,’Kichaka’ na ‘Maria Salome’ ambayo ilimuweka vyema katika uliomwengu wa muziki ameahidi kufanya vyema katika tamasha hilo.

“Nimefurahi sana kupata bahati ya kuperform Sauti za Busara kwa mara nyingine, Sauti za Busara nimeshawahi kwenda  kushiriki mwaka 2005 na leo naenda kushiriki mwaka 2018. Ni miaka mingi na ndio maana wanasema nimepotea  lakini nashukuru tena kunipokea  na kunifanya ninyanyuke mara nyingine tena,” amesema msanii huyo.

Pia akasisitiza “Sauti za Busara ni sehemu nzuri ya kukutana na wenzetu na kubadilishana mawazo, kuonana na wenzetu  tukabadilishana fikra na vilevile nyimbo zetu ni kwa ajili ya kuondoa mawazo kwenye vichwa vyetu.”

Tamasha la Sauti za Busara ufanyika kila mwaka mwezi wa pili, na hukutanisha wasanii tofauti tofauti katika muziki. Tamasha hili ufanyika kisiwani Zanzibar na limekuwa tamasha la kuvuta hisia za watu kwani muziki unakuwa Live.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents