Michezo

Kyle Edmund atinga nusu fainali ya Australian Open

Mchezaji tennis,Kyle Edmund ameendeleza ubabe wake katika michuano ya Australian Open baada ya kumshinda Grigor Dimitrov na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali nakuwa Grand Slam yake ya kwanza kufika hatua hiyo.

Katika mchezo huo uliyopigwa katika dimba la Rod Laver Arena, Edmund mwenye umri wa miaka 23, ameshinda kwa jumla ya seti 6-4 3-6 6-3 6-4 ndani ya masaa mawili na dakika.

Kyle Edmund ambaye anashika nafasi ya pili katika viwango vya ubora wa mchezo huo nchini Uingereza huwenda akakutana na muingereza mwenzake Andy Murray ambaye anashika nafasi ya kwanza nchini humo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents