Habari

Sakata la Ozil kujiuzulu kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani, Lashusha neema nchini Uturuki

Sakata la kiungo mshambuliaji wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani, Mesut Ozil kujiuzulu kuitumikia timu yake ya taifa limeleta sura mpya ya mapatano ya kibiashara kati ya Ujerumani na Uturuki.

Image result for ozil and erdogan
Mesut Ozil akiwa na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan

Serikali ya Ujerumani kupitia taarifa iliyochapishwa na gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung imeeleza kuwa imeondoa vikwazo vyote vya kibiashara ambavyo ilikuwa imeiwekea Uturuki tangu mwaka juzi.

Waziri wa Nishati na Uchumi nchini Ujerumani, Peter Altmaier amesema kuwa maamuzi ya serikali yamekuja baada ya Uturuki kuondoa hali ya hatari iliyodumu kwa mwaka mmoja tangu litokee jaribio la kutaka kumpindua Rais wa hiyo, Recep Tayyip Erdogan.

Uturuki  inaingiza zaidi ya dola bilioni $1.7 kwa mwaka kwa kuuza bidhaa zake nchini Ujerumani.

Maamuzi hayo pia yamekuja siku moja baada ya Mesut Ozil (Mjerumani mwenye asili ya Uturuki) kutangaza kuwa ameacha kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani kwa kile alichozungumza kuwa anabaguliwa na hapewi heshima na Shirikisho la soka nchini Ujerumani (DfB) .

Ozil amesema kuwa alikuwa anaandamwa na vyombo vya habari na mashabiki baada ya kupiga picha mwezi Mei mwaka huu akiwa na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan na kueleza kuwa mara nyingi timu ya Ujerumani ikishinda anaitwa Mjerumani lakini ikipoteza anaitwa mkimbizi kutoka Uturuki .

Kitendo cha Ozil kupiga picha na Erdogan kilichukuliwa kuwa cha kisiasa na ukizingatia kipindi hicho Uturuki ilikuwa kwenye uchaguzi Mkuu wa Urais ambapo Erdogan alishinda kwa kishindo.

Rais Recep Tayyip Erdogan bado anatajwa kama Rais mwenye vina saba vya Udikteta nchini Uturuki na mataifa kibao barani Ulaya yamekuwa yakimuonya kwa vitendo vyake vya kukiuka haki za kibinadamu.

Related Articles

One Comment

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents