BurudaniHabari

Sanamu la Kobe Bryant lazinduliwa, la kwanza kati ya matatu

Klabu ya kikapu ya Los Angeles Lakers wameonyesha heahima kubwa kwa Kobe Bryant kwa kuamua Kimjemgea Sanamu katika Uwanja wao wa Lakers huko Los Angeles .

Sanamu hilo la Kobe Bryant limezindiliwa na Mjane Vanessa siku ya Alhamisi hii ishara ya kumpa heshima kubwa nyota wao marehemu kwa sura yake kwa Sanamu hilo lenye urefu wa futi 19 nje ya uwanja wao.

Sanamu hiyo inamuonyesha Bryant katika jezi yake nyeupe nambari 8 huku kidole chake cha shahada cha kulia kikiwa kimeinuliwa Juu ishara aliyoitumia wakati walipopata matokeo ya pointi 81 dhidi ya Toronto Raptors Januari 2006.

Mjane wa Bryant, Vanessa, alipewa heshima kubwa ya kuzindua Sanamu hilo huku akitoa ujumbe wakati wa hafla ya kuwekwa wakfu kuwa sanamu hiyo ni ya kwanza kati ya matatu ambayo yanatarajiwa kujemga kama Ishara ya Heshima kwa Legend huyo ya mpira wa kikapu ili kumuenzi bingwa huyo mara tano wa NBA na mfungaji bora katika historia ya Lakers.

Sanamu nyingine itamwonyesha Bryant katika jezi yake nambari 24, ambayo aliivaa kwa kipindi cha pili cha maisha yake ya soka, huku ya tatu ikiwa ni picha ya Bryant na binti yake, Gianna, aliyefariki pamoja naye na wengine saba katika ajali ya helikopta Januari 2020.

link ya video ipo chini hapa..!

https://www.instagram.com/reel/C3HRSW4tAVE/?igsh=MW11dzdtcGN4aWpoYw==

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents