Habari

Serikali haizuii harakati za kisiasa – Mh. Antony Mavunde

Serikali imesema kuwa si kweli kwamba inazuia harakati za kisiasa.

Akijibu kwa Niaba ya Waziri Mkuu, leo Mei 7 Bungeni jijini Dodoma Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde wakati akijibu swali la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini alihoji,

Sheria ya vyama vya siasa imeweka masharti ya wazi na yaliyokamilika ya namna ambavyo vyama vitapata wanachama wake na vitaeleza sera na itikadi yake lakini kwasasa sasa Polisi wamekuwa na desturi ya kuzuia vikao vya vyama vya siasa hata vikao vya ndani vinavyopanga uenezi wa chama, sasa serikali haioni kwamba baada ya kusimamia sheria serikali yenyewe kwa kutumia vyombo vyake ina vunja sheria na kama inataka hayo masharti ya sasa yaendelee ilete sheria hapa bungeni ili kuweza kuweka hayo masharti mapya badala ya kutumika kuwapiga wanasiasa mitaani?

Si kweli kamba serikali inazuia harakati za kisiasa na hata sheria aliyoisema Mh. M/Kiti sheria hii imetoa uhuru kwa vyama kutafuta wanachama nakufanya mikutano, lakini iko subject na sheria zinginezo ikiwepo sheria ya policy force ya service act ambayo imeweka masharti katika section namba 44 /45 ya namba ya vyama vya siasa inaweza ikafanya nikutano na katika maandamano mbalimbali ,” – Mh. Antony Mavunde

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents