Habari

Serikali imemfungia msanii Wema Sepetu kutojihusisha na filamu kwa muda usiojulikana (+Video)

Serikali imemfungia msanii Wema Sepetu kutojihusisha na filamu kwa muda usiojulikana

Msanii wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu leo baada ya kuitwa kuhojiwa na Bodi ya Filamu Tanzania kuhusu kusambaa kwa picha zake za faragha kwenye mitandao ya kijamii, Imeamua kumfungia msanii huyo kujishughulisha na mambo ya filamu.

Bodi hiyo imeamua  kumfungia msanii huyo na kumtaka kutojishughulisha na filamu kwa muda usiojulikana, kufuatia picha zake chafu zilizosambaa mtandaoni.

Ikubukwe kwamba msanii huyo aliomba msamaha siku ya jana kutokana na tukio hilo ambalo lilitokea siku kadhaa nyuma ambayo alionekana akiliwa denda na mwanaume anayesemekana ni raia wa Burundi.

Wema amekuwa akijihusisha mara kwa mara na matukio ya kusambaza picha zisizo na maadili mitandaoni na amekuwa akionywa na vyombo husika lakini mara hii vimeamua kumfungia kabisa kutojihusisha na mambo ya filamu.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents