Habari

Serikali kuchukua hatua kuhakikisha riba za mikopo benki zinapungua

Serikali imesema kuwa pamoja na huduma za bidhaa ya fedha kuamuliwa na nguvu ya soko kwa upande wake imekuwa ikichua hatua za kisera ili kuhakikisha kuwa riba za mikopo zinapungua katika soko hapa nchini.

Hayo yameelezwa Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango,Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Konde, Khatibu Haji aliyehoji, Serikali inachukua hatua gani ili benki ziweze kupunguza viwango hivyo vya riba?

“Baadhi ya hatua zilizochukuliwa na Serikali kupitia Benki Kuu ni pamoja na kuzitaka benki za biashara kutumia mfumo wa kuhifadhi na kutoa taarifa za wakopaji (Credit Reference Bureau System). Aidha, Benki hiyo imekuwa ikitoa mikopo ya muda mfupi kwa benki za biashara kwa kiwango cha asilimia 6.89,” alisema Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji alizitaja hatua nyingine zilizochukuliwa kuwa ni Benki Kuu kushusha riba (Discount Rate) kutoka asilimia 16.0 hadi asilimia 9.0 pamoja na kupunguza kiwango cha chini cha amana kinachotakiwa kuwekwa Benki Kuu na benki za biashara (Statutory Minimum Reserve Requirememnt (SMR)) kutoka asilimia 10.0 hadi asilimia 8.0.

Aidha, amesema baada ya hatua hizo za kisera kuchukuliwa na Serikali, baadhi ya benki za biashara hapa nchini zimeanza kupunguza riba za mikopo.

Ameongeza kuwa, Serikali itaendelea kuchukua hatua za kisera ili kuhakikisha kuwa riba za mikopo katika soko zinaendelea kupungua.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents