Habari

Serikali yaahidi kuwashushia neema watumishi wake

Serikali imesema itaboresha mishahara ya watumishi wa umma mara baada ya kukamilika kwa zoezi la kuwabaini wafanyakazi hewa katika idara za serikali.

waziri-mkuu-kassim-majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, pia amesema serikali itaondoa malimbikizo ya mishahara kwa watumishi stahiki.

“Nafahamu kuwa yapo madai mbalimbali yakiwemo malimbikizo ya mishahara kwa watumishi. Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuhakikisha kwamba tunaondoa malimbikizo ya madai kwa watumishi wote wa umma. Moja wapo ni kuanza kuhakikisha azma hii ni pamoja na kuanza kufanya uhakiki wa taarifa za kiutumishi kwa watumishi wa umma ili kubaini watumishi hewa. Ni zoezi ambalo bado linaendelea kwa sasa na limesaidia pia kubaini watumishi wa umma hewa wapatao 16,500 kufikia tarehe 20 mwezi huu wa 10,” alisema Majaliwa.

“Baada ya zoezi hilo tutarudia uhakiki wa madeni yote yaliyowasilishwa serikalini ya wale watumishi stahiki ili kuweza kujua madai halisi na tuanze kuyalipa.”

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents