Habari

Serikali yaanza kufanyia kazi maoni na malalamiko ya kodi

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango amesema kuwa serikali imeanza kuyafanyia kazi maoni na malalamiko ya wafanyabiashara na wawekezaji juu ya kodi zinazolalamikiwa kwa lengo la kubadili kodi zinazoonekana kuwa ni kero.


Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Philip Mpango.

Dkt Mpango ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea na kukagua maonesho ya kwanza ya viwanda vya Tanzania yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kutoa wito kwa wafanya biashara na wawekezaji kuwasilisha maoni yao kuanzia mwezi huu.

“Mwezi huu natangaza wizara ya fedha, natangaza kwa umma mtu yeyote ambaye ana mawazo, ana ushauri, ana malalamiko juu ya kodi ya aina yeyote ailete kwangu kwasababu sasa hivi ndiyo tunaanza utaratibu wa kupanga kodi na vyanzo vya mapato kwaajili ya mwaka ujao wa fedha kwahiyo hiyo ni fursa. Maana kodi zina utaratibu wa kisheria siwezi kubadilisha kitu ambacho tumekiweka kisheria kwa sasa,” alisema Mpango.

Aidha waziri Mpango ametoa wito kwa Watanzania kujenga tabia na utamaduni wa kuthamini na kununua bidhaa zinazotengenezwa nchini ili kujenga uchumi wa ndani badala ya kununua bidhaa kutoka nje ya nchi ambavyo vingi kwa sasa vinazidiwa ubora na bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents