Habari

Serikali yakabidhiwa uwanja wa Uhuru baada ya ukarabati kukamilika

Serikali imekabidhiwa rasmi uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam baada ya ukarabati mkubwa kukamilika.

5R5A9295

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye,amepokea uwanja huo kwa niaba ya serikali na kuwapongeza wakandarasi ambao ni kampuni ya China ya Beijing Construction Engineering Group Company Limited (BCEG) na mshauri mwelekezi wa uwanja huo kampuni ya kizalendo chini ya uongozi wake, Injinia Aloyce Peter Mushi kwa kazi nzuri iliyofanyika licha ya mikwamo ya hapa na pale.

5R5A9556

“Ndugu zetu Wachina, wameonyesha sio tu uhusiano mzuri bali wameonyesha kuwa wao ni ndugu zetu, kwani walishiriki wakati nchi yetu ikipata uhuru lakini toka wakati huo hadi hivi sasa, bado wanashiriki katika kusaidia kuimarisha uchumi wetu,” alisema Nnauye.

Waziri Nnauye aliwataka watumiaji wa uwanja huo kulipa ada za matumizi kama inavyostahili, ili hatimaye fedha hizo ziweze kugharimia matunzo ya uwanja.

5R5A9255

Mshauri huyo mwelekezi wa ujenzi huo, Injinia Aloyce Peter Mushi alisema, uwanja huo una uwezo wa kuchukua watu elfu 22 na ulikamilika na kuanza kutumika kwa mara ya kwanza Mei 22, 2015.

5R5A9577
Injinia Aloyce Peter Mushi

Meneja Mkuu wa Kampuni ya BCAG, Cheng Long Hai, aliweza kutoa sifa za uwanja huo kuwa umewekewa mifumo yote muhimu kama vile tanki la kuhifadhia maji na mifumo ya maji taka, na kuishukuru serikali ya Tanzania kwa kuiamini kampuni yake kutekeleza mradi huo mkubwa.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents