Habari

Serikali yataja adui namba moja wa viwanda

Serikali imesema adui namba moja wa viwanda nchini ni bidhaa bandia na zile zisizo kidhi viwango.

Akijibu kwa niaba Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Dkt Isack Kamwelwe leo bungeni, mjini Dodoma akijibu swali la mbunge alietaka kujua serikali inachukua hatua gani juu ya kudhibiti bidhaa bandia nchini?

“Serikali inaendelea kudhibiti bidhaa bandia zisiingie nchini ili kuhakikisha ushindani wa haki katika biashara, katika kipindi cha Januari hadi Disemba mwaka 2016 tume ya ushindani ili kamata bidhaa bandia zenye thamani ya shilingi bilioni 18. 67 bidhaa hizo zilikamatwa kwenye kaguzi za bandarini, vitengo vya Makontena na katika Masoko, kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Machi 2017 shirika la viwango Tanzania TBS kwa kushirikiana na Taasisi nyingine waliteketeza bidhaa mbalimbali zenye thamani ya shilingi bilioni 2.4,” amesema Kamwelwe.

“Bidhaa hizo ni pamoja na nguo, nyama na soseji, vilainishi vya injili,betri za magari, shirika pia lilifanya ukaguzi wa mabasti na kuteteketeza mabati 84,000 ambayo hayakukidhi viwango Tumeya ushindani na TBS ziendelee kushirikiana na taasisi nyingine kudhibiti bihaa zinazoingia katika mipaka nchi jirani kufuatilia ubora wa bidhaa hafifu na za bandia na kuziondoa katika soko. waheshimiwa wabunge na wananchi wote tushirikiane kutokomeza bidhaa bandia na zisizo kidhi viwango. Adui namba moja wa viwanda ni bidhaa bandia, na zile zisizo kidhi viwango.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents