Burudani

Shetta kubonga na wateja wa Vodacom ‘LIVE’

Mashabiki wa mwanamuziki wa kizazi kipya wa bongo fleva Nurdin Billal alimaarufu kama Shetta watapata fursa ya kubonga naye Live Kutokana na kuzinduliwa kwa huduma mpya ya ‘Bonga na Star’ iliyozinduliwa leo na Vodacom Tanzania mahususi kwa wateja wake.

002.chat
Shetta (katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na kupata fursa ya kwanza ya kuongea moja kwa moja “LIVE” na mashabiki wake ambao ni wateja wanaotumia mtandao wa Vodacom Tanzania.Ili kujiunga na huduma hiyo mteja anatakiwa kupiga namba 0901766666 na kujiunga kwa shilingi 150 na atakapokuwa ameunganishwa na kuanza kuongea na Staa atakatwa shilingi 20 kwa dakika.Wengine katika picha ni Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Matina Nkurlu(kushoto)na Mathew Kampambe ambaye ni Meneja wa huduma za ziada

Huduma hii ni kwa ajili ya wateja wote wanaotumia mtandao wa Vodacom inawawezesha kuunganishwa na mastaa maarufu wanaowashabikia na kuweza kuongea nao moja kwa moja kupitia simu zao za mkononi katika siku maalumu zitakazokuwa zinapangwa na wateja kupatiwa taarifa kupitia simu zao za mkononi.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hii ya aina yake Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu alisema kuwa kwa mara nyingine tena Vodacom imekuja na huduma ya kuleta furaha kwa wateja wake itakayowapatia fursa ya kuongea live na mastaa wanaowashabikia.

“Kwa mara nyingine tena Vodacom tumewaletea promosheni hii ya aina yake ya kuwaletea furaha wateja wetu ukiwa na mwendelezo wa huduma mbalimbali za hapo awali ingawa hii ni tofauti kidogo kwa kuwa inawawezesha wateja wetu kuongea na mastaa wanaowashabikia Live ambapo wanaunganishwa nao na kuongea nao kwa gharama nafuu.

“Hii itafanyika katika siku maalumu zitakazopangwa ambapo wateja watakuwa wanafahamishwa mtu maarufu atakayekuwa amepangwa kabla ya siku kupitia simu zao na kwenye vyombo vya habari,” alisema Nkurlu.

Nkurlu aliongeza kusema, “Mastaa maarufu wenye washabiki wapo wa makundi mbalimbali wanaweza kuwa wachezaji wa mpira na michezo mingine,wanamuziki,wacheza sinema,wasanii wa maigizo na wengineo kinachotakiwa ili kuelewa jinsi ya kushiriki katika promosheni hii anachotakiwa kufanya mteja ni kununua tiketi ya kushiriki kupitia simu namba 0901766666 na kuunganishwa na huduma hii kupitia simu hiyohiyo na kuongea na msaniii anayemshabikia kwa dakika moja.”

Alisema kwa anayehitaji kupata huduma hii anatozwa kiasi cha shilingi 150 ya kununua tiketi ili aunganishwe na shilingi 20 kwa kila dakika ya maongezi ambazo zinakatwa kutoka muda wa maongezi wa mtumiaji wa huduma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents