Burudani

Shilingi milioni 15 zimetumika kushoot video mpya ya Hemedy PHD katika mikoa minne

Hemedy PHD anakuja na video yenye utofauti mkubwa. Video ya wimbo wake ‘Imebaki Story’ imefanyika kwenye mikoa minne nchini.

AvdtTr1kDJVhy2IXaiTIHfgEub5a-TZ0GGFTq--rijKk

Video ya wimbo huo uliotayarishwa Sei Records imefanywa na Kwetu Studios itatoka July 30. “I am still proud kushoot bongo sababu locations kali tunazo,” Hemedy ameiambia Bongo5.

“Nahamasisha wasanii wenzangu kutumia more nyumbani na kupatangaza pia,” ameongeza.

Amesema video hiyo imefanyika kwenye mikoa ya Arusha, Morogoro, Dar es Salaam na Manyara na kwamba imemgharimu takriban shilingi milioni 15.

“Thank God niliweka malengo ya kufanya kitu kizuri home, nafikiri ni video yenye kiwango kizuri na inaitangaza Tanzania pia sababu nimetumia sehemu kubwa kuonyesha uzuri wa nchi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents