Burudani

Shilole adai ametumia shilingi milioni 60 mpaka sasa kwenye ujenzi wa nyumba yake

Msanii wa muziki na filamu Shilole, amesema kuwa mpaka sasa hivi ametumia kiasi cha kati ya shilingi milioni 45 mpaka 60 katika ujenzi wa nyumba yake anayomalizia huko Kimara, Dar es salaam.

Nyumba ya mwanadada shilole.
Nyumba ya mwanadada shilole.

Akizungumza na Clouds FM hivi kazibuni, Shilole amesema ujenzi wa nyumba yake umetumia miaka miwili mpaka sasa na bado haijakamilika.

“Nyumba yangu ipo hatua ya mwisho,na nimeshatumia kati ya milioni 45 mpaka 60 na bado maridisha ,milango, tires na umeme ,mungu alinijalia nitaimalizi taratibu”Alisema Shilole.

Pia Shilole amesema ameamua kujenga nyumba ili kuwatengenezea mazingira mazuri watoto wake wasije wakateseka hapo baadae hapa mjini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents