Burudani

Sijawahi kuumizwa kwenye mapenzi – Ditto

Msanii wa muziki, Lameck Ditto ambaye pia ni baba wa mtoto mmoja amedai katika maisha yake ya mahusiano ya mapenzi hajawahi kuumizwa.

Ditto

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Moyo Sukuma Damu’ amesema kwa sasa anaishi na mama watoto wake.

“Mimi kwenye mahusiano ya mapenzi sijawahi kuumizwa,” Lameck alikiambia King FM. “Kwenye mahusiano mimi ni baba wa mtoto mmoja, nimempata mzazi mwenzangu ambaye anaishi naye. Mtoto wangu Lameck ana miaka 2 na kusema kweli tunafurahia maisha yetu na mungu akijalia tutafunga ndoa,”

Muimbaji huyo ambaye pia ni mfanyabishara wa kilimo amekuwa ni mmoja kati ya wasanii ambao hawategemei kiki kwenye muziki wao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents