Burudani

Siku ya Vijana: Wasanii na wadau wengine waizungumzia Tanzania ijayo (Picha)

Wasanii wa muziki, filamu pamoja wa wanamitindo hapa nchini jana waliungana na wadau mbalimbali kuadhimisha siku ya vijana duniani kwa kujaliana kuhusu Tanzania ijayo ndani ya mdahalo uliopewa jina la ‘Ndoto Kubwa’.

Humphrey Polepole akifanua jambo
Humphrey Polepole akifanua jambo

Wakizungumza kwenye mdahalo huo uliofanyika kwenye ukumbi wa New Africa Hotel jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na taasisi ya Tanzania Bora Initiative, vijana hao walieleza mambo mbalimbali ya kuzingatia ili kukuza uchumi wa nchini.

Rapper Nickwa Pili ambaye aliyekuwa msemaji mkuu alizungumzia kuhusu maadili ya viongozi.

“Nimesikia mtu anasema maadili, hatuna maadili hatuna nini lakini tukumbuke mfumo wa uchumi unatengeneza aina ya maadili. Mimi mfumo wa Dar es salaam hauniruhusu kukaa vyumba vitatu, ninaweza ku- afford kulipia vyumba viwili. Pia kama tunaongelea maadili ya viongozi, viongozi wamezaliwa na mfumo wa pesa, demokrasia ni mfumo wa pesa, inabidi uwe na pesa za kuhonga watu, ili uwe rais unatakiwa kuwa na pesa za kufanyia kampeni, kwahiyo lazima tujibu maswali haya magumu halafu ndio tuende kwenye maadili,” alisema rapper huyo.

Kwa upande wake muigizaji wa filamu, Rose Ndauka aliwakata waandishi wa habari kuhakikisha wanapeleka ujumbe sahihi kwa watanzania bila kupindisha.

“Mimi nawataka waandishi wa habari au watu ambao wanawafikishia watu wengine habari ambazo zinazungumziwa. Sisi hapa tulipo ni wachache sana lakini naamini kuna watu watapeleka habari sehemu nyingine kwa vitu tulivyozungumzia hapa, sasa wale ambao mnapeleka habari unaendaje kuwasaidia vijana au watu walio nje ili kumchagua kiongozi aliyE bora? Mnaenda kuandika maneno gani? Kwahiyo tuangalie hata wenye vyombo vya habari vitu gani mnaandika kuwasaidia watanzania na sio kuharibu na sio kwa benefit zao wenyewe,” alisema Rose.

Wachangiaji wakuu wengine walikuwa ni pamoja na Humphrey Polepole ambaye ni mjumbe wa tume ya mabadiliko ya katiba na Emelda Mwamanga.

Emelda Mwamanga akizungumza jambo
Emelda Mwamanga akizungumza jambo

Modesta Lilian Mahiga  akizungumza katika mdahalo huo
Modesta Lilian Mahiga akizungumza katika mdahalo huo

Mmoja kati ya waanshilishi wa Tanzaniabora Initiative, Godfrey Nyombi
Mmoja kati ya waanzilishi wa Tanzania Bora Initiative, Godfrey Nyombi

Mwongozaji wa mdahalo Rebecca Gyuni
Mwongozaji wa mdahalo akiwa kazini

Burudani ikiongozwa na Mwasiti Almas
Burudani ikiongozwa na Mwasiti Almas

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents