Habari

Simbachawene aingilia kati mgogoro wa ardhi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amewataka wananchi wa Kitongoji cha Chihikwi, Kata ya Mbarawara, Jijini Dodoma, kusubiri majibu ya Serikali kuhusu mgogoro wa ardhi uliopo baina  yao na Jeshi la Magereza.

Mgogoro huo wa ardhi kati ya Wananchi na Jeshi la Magereza umedumu kwa miaka nane,hali iliyomlazimu Mh.Simbachawene kuzuru eneo hilo kwa lengo la kuzungumza na Wananchi hao na kusikiliza kero zao.

Baada ya kuzungumza na wananchi ,Waziri Simbachawene amesema ataenda kutafakari na kuyafanyia kazi kero na malalamiko yote yaliyozungumzwa na atarudi kwa niaba ya serikali kutoa majibu na watazingatia umuhimu wa kila upande.

Aidha,Mh.Simbachawene amesema licha ya kuwa anatarajia kuja na majibu ya maoni hayo lakini wananchi hao wanapaswa kujua kuwa ardhi ni mali ya umma, kama Serikali inaweza ikaichukua ardhi kwa ajili ya masuala ya umma na wananchi wanapaswa kupisha kufanya shughuli yake na pia haki ya mwananchi kulipwa fidia kwa kile alichokiendeleza katika ardhi na siyo vinginevyo.

“Nimesikia maoni yenu lakini lazima niende nikatafakari, nitahakikisha mimi mwenyewe nitarudi hapa hapa katika mti huu huu kutoa majibu, mapema iwezekanavyo, nafahamu kabisa kamati ya kufuatilia mgogoro huu ilifanya kazi kubwa na mlikuwa na wawakilishi wenu, tufikirie kumaliza huu mgogoro ili shughuli zingine ziendelee,” alisema Simbachawene.

By-BAKARI WAZIRI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents