Habari

Sirudi CCM hata kama nateseka – Mhe Frederick Sumaye

Waziri mkuu mstaafu wa Tanzania, Mhe Frederick Sumaye, amedai hashangazwi na mateso na manyanyaso anayoyapata kwa sasa, kwani aliyajua hayo tangu alipoamua kuhama CCM, na kutimkia upinzani.

Mhe Frederick Sumaye

Mhe Sumaye amesema kuwa kuna watu waliahidi kumfilisi mali zake yakiwemo mashamba yake mapema alivyotangaza kuungana na upinzani mwaka 2015 .

“Nilipoingia tu kwenye upinzani mwaka 2015 wakati wa kampeni wapo baadhi ya viongozi walitamka wazi kuwa huyu adhabu yake ni kumnyang’anya mali zake mpaka aw masikini, kwahiyo nilitegemea hayo yangetokea tu kama adhabu kwa sababu nilihamia kwenye upinzani”,amesema Mhe Sumaye.

Hata hivyo Mhe Sumaye amesema kuwa hawezi kurudi CCM hata kama wangemtesa na kumfilisi mali zake zote kwani alijipanga hata kabla ya kujiunga na upinzani.

“Kama wanafikiria mimi nitarudi CCM kwa kuteswa? nasema sirudi CCM heti kwa sababu nateseka”,amesema Mhe Sumaye kwenye mahojiano yake na Azam TV.

Kwa upande mwingine Mhe Sumaye ameishauri serikali kunyang’anya mashamba kwa watu walioshindwa kuyaendeleza na sio kwa sababu za kisiasa.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents