Habari

Soggy Doggy aeleza jinsi wimbo wake ulivyotumika kwenye filamu ‘Sometimes in April’ ya Idris Elba na kutolipwa hata senti

Sometimes in April ni filamu ya mwaka 2005 iliyoigizwa kuelezea mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda ya mwaka 1994.

article-2349925-1A83A6EF000005DC-292_634x475
Muigizaji raia wa Uingereza, Idris Elba aliigiza kama Augustin Muganza kwenye filamu hiyo

Iliandikwa na kuongozwa na mtengenezaji wa filamu wa nchini Haiti Raoul Peck na kuchezwa na waigizaji kama Idris Elba, Oris Erhuero, Carole Karemera na Debra Winger.

Kwa wengi ambao hawajaiona filamu hiyo hawafahamu kama wimbo wa rapper Soggy Doggy ulitumika kwenye filamu hiyo.

“Ile movie ilichezwa na Wamarekani pamoja na wasouth Africa,” Soggy alieleza segment ya ‘Chumba cha Sindano’ ya kipindi cha Kali za Bomba kupitia kituo cha redio cha Bomba FM 104.0, cha Mbeya.

http://www.youtube.com/watch?v=XiteY6o2UwI

“Mwanzoni pale ikianza kuna wimbo wangu mimi na Dataz ambao ulikuwa unaitwa ‘Sikutaki Tena’. Sasa mpaka leo hii jiulize ni nani aliyeuchukua ule wimbo akaenda akawapelekea wale Wamarekani, wakautumia kwenye ile filamu hadi filamu ikavunja rekodi ya mauzo katika movie ambazo zinaelezea vitu halisi ya vita vya Afrika. Lakini tuulize sisi tulipata nini, tuulize ni nani aliyepeleka ule wimbo. Kutakuwa kuna Mtanzania mmoja mwenye akili kubwa kuliko Soggy na Dataz ambaye aliamua kuuchukua ule wimbo na kwenda kufanyia biashara naye akaendelea kunufainika sisi tukaendelea kuwa maskini.”

Msikilize zaidi Soggy hapa.

[soundcloud url=”http://api.soundcloud.com/tracks/112379990″ params=”” width=” 100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents