Burudani

Soulja Boy aweka hadharani verse iliyofutwa na Kanye West kwenye ngoma ya ‘Remote Control’ (+ Video)

Soulja Boy anaendelea kumtupia lawama Kanye West baada ya kutoa verse zake kwenye ngoma ya “REMOTE CONTROL” inayopatikana kwenye album ya DONDA iliyotoka siku ya Jumapili.

Soulja Boy kupitia mtandao wake wa Tweet alisema”ni muda mwingi nimepoteza na wewe studioa si Bora huo muda ningetengeneza album yangu” pia Soulja Boy aliamua kuposti kwenye Instagram kipande cha video ambacho zinasikika verse zake ambazo zilikuwa kwenye ngoma ya “REMOTE CONTROL” kabla ya kutolewa na aliamua kuvujisha baadhi ya meseji alizokuwa akichati na Kanye kabla ya kwenda kurekodi nae ngoma hiyo ya “REMOTE CONTROL” hata hivyo sio Soulja Boy pekee yake anayelalamika verse zake kufutwa Bali hata Chris Brown ni miongoni mwa wasanii ambao Kanye aliwatema kwenye album hiyo

Album ya DONDA ina jumla ya Nyimbo 27 na amewashirikisha vichwa Kama Jay Z, Roddy Rich,Lil Baby,Travis Scott,The Weekend,Pop Smoke,Don Toliver,Lil Yachty,Lil Durk pamoja na Young Thug,Mpaka sasa album ya DONDA imeweka rekodi ya kuwa ndio album ilisikilzwa sana ndani ya siku moja,mpaka sasa inakamata namba moja kwenye Apple music kwenye nchi zaidi ya 130 Duniani kote.

Bofya hapa chini kutazama.

 

https://www.instagram.com/p/CTPS_kUj433/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents