Burudani

Stopa adai muziki wa Tanzania umeingiliwa na ‘mdudu rushwa’ na ushikaji

Msanii kutoka pande za Arusha Stopa Rhymes amedai kuwa muziki wa Tanzania umeingiwa na mdudu rushwa na ushikaji hali ambayo inawaathiri wasanii wengi.
stoppa

Stopa ameiambia Bongo5 kuwa unaweza ukaumiza sana kichwa kwenye kuandaa mashari lakini ukatoka patupu kutokana na muundo wa muziki wa sasa.

“Kuna wakati unafikia na unajiuliza huu muziki ukoje,unaandika mashairi unaumiza kichwa lakini unakuta tofauti na wanavyoupokea watu na muziki wa Tanzania sasa hivi umeingiwa na mdudu ushikaji na kitu kimoja kinaitwa rushwa,kwahiyo muziki wa Tanzania sasa hivi umeingiliwa na rushwa na ushikaji ndio kitu ambacho kinaudhoofisha muziki wetu pamoja na wasanii,” alisema.

Pia amedai kuwa baada ya kuona muziki umekuwa ndivyo sivyo amejipanga na kuanzisha biashara ndogo ndogo ambazo zinatokana na muziki wake.

“Biashara ya t-shirt na album zimenisaidia sana,nimekuwa nikituma katika mikoa mbalimbali na mauzo kusema kweli yanatia moyo sana na zinaweza zikakuendeshea maisha yako vizuri tofauti hata na pesa za show ambazo sometimes zimakuwa za majungu,kwamba unatangazika lakini unachokipata ni kidogo,kwahiyo nitaendeleza harakati za muziki na huku nikifanya biashara ya t-shirt pamoja na album za muziki wangu ambazo natoa.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents